Gigy Money Awaponza Wasafi, TCRA Yawafungia Miezi 6

 

Gigy Money Awaponza Wasafi, TCRA Yawafungia Miezi 6

Gigy Money Awaponza Wasafi, TCRA Yawafungia Miezi 6

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeifungia Televisheni ya Wasafi TV kutoa huduma kwa muda wa miezi sita kuanzia Januari 6, 2021, hadi Juni 2021 kwa makosa ya kukiuka taratibu za utangazaji.

 

Maamuzi hayo yanakuja kufuatia maudhui ya picha jongefu yaliyomwonesha msanii wa Bongo, Fleva, Gift Stanford, maarufu kama Gigy Money akicheza utupu kinyume na kanuni za maadili katika tamasha la Tumewasha Live Concert lililorushwa Januari Mosi 2021 kuanzia saa mbili hadi saa tano usiku.

 

Aidha Wasafi TV wanatakiwa kutumia siku ya leo kuomba radhi kwa watazamaji wake kufuatia ukiukaji huo na wakikaidi hatua zaidi za kisheria na udhibiti zitachukuliwa.

Gigy Money afungiwa na kupigwa faini


Gigy Money afungiwa na kupigwa faini


Leo December 5, 2020 Baraza la Sanaa Taifa ( BASATA ) limemfungia miezi sita msanii wa muziki ‘Gigy Money kutojushughulisha na shughuli zozote za muziki.

Katika taarifa yao, Basata imeeleza kuwa imefikia hatua hiyo baada ya msanii huyo kuvaa nguo zisizo na maadili katika Tamasha la Wasafi ililofanyia Alhamisi iliyopita jijini Dodoma, hivyo kukiuka kanuni za kifungu cha 4(L) cha sheria namba .23 ya mwaka 1984.

Basata imesema adhabu hiyo inaendana na faini ya Sh milioni moja na kwamba adhabu hiyo imezingatia kanuni ya 64 (1)( a)-(i) za Baraza la Sanaa Tanzania mwaka 2018.

ANGALIA TAARIFA KAMILI KUPITIA VIDEO HII

👇👇👇👇👇👇👇👇👇JIUNGE NASI KWENYE GROUP LETU LA WHATSAPP HAPA
👇👇👇👇👇👇
www.juniortvtz.com

Post a Comment

1 Comments