Kagere Amkataa ‘Baba Yake’


Kagere Amkataa ‘Baba Yake’

MSHAMBULIAJI wa Simba, raia wa Rwanda, Meddie Kagere, ameibuka na kusema kuwa, yeye si Mtanzania na hamtambui mzee anayesema ni baba yake.

 

Hivi karibuni, mzee Vedasto Katologi, aliliambia Championi kuwa, Kagere ni mwanawe na kama kuna mtu anabisha, basi yupo tayari kwenda kupima DNA ili kujiridhisha.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kagere alisema: “Eti kuna mtu anasema yeye ni baba yangu? Hapana, sina taarifa hizo na sijawahi kuongea naye, aache uzushi, mimi sina undugu naye.”

 

Kagere aliyejiunga na Simba msimu wa 2017/18 akitokea Gor Mahia ya Kenya, huu ni msimu wake wa tatu ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa kinara wa ufungaji katika ligi hiyo kwa misimu miwili mfululizo.


Toa Maoni yako hapa msomaji wetu.....JIUNGE NASI KWENYE GROUP LETU LA WHATSAPP HAPA
👇👇👇👇👇👇
www.juniortvtz.com


 

Post a Comment

0 Comments