Ajali Ya Treni Iliyokua inatoka Dar Kuelekea Bara - Kigoma

Ajali Ya Treni Iliyokua inatoka Dar Kuelekea Bara

 Treni ya abiria iliyokuwa inatoka Dar Es Salaam kuelekea Bara (Mwanza, Mpanda na Kigoma kupitia Tabora) imepata ajali Wilayani Bahi umbali wa KM 40 kutoka Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amethibitisha.

"Treni ilikuwa na Watu zaidi ya 700,  kuna mvua zinanyesha sana, bado hatujajua chanzo cha ajali ila kichwa kimeanguka, taarifa za awali zinaonesha Mfanyakazi wetu mmoja amefariki na abiria wawili wamefariki, nilikuwa likizo nimeikatisha naelekea eneo la tukio”- Kadogosa

"Tunaandaa Mabasi ya kwenda kuchukua abiria pale wawapeleke Manyoni, kuna Treni yetu ya abiria inatoka Bara, wanaoendelea na usafiri Bara waingie huko waendelee na safari, na waliokuwa wanatoka Bara kuelekea Dar Es Salaam waingie kwenye Mabasi wawalete DSM"-Kadogosa


Baadhi ya TAARIFA Zilizo tufikia Ni hizo

Na huu ndio ujumbe ambao unasambazwa MDA huu kwenye magroup ya WhatsApp 

👇👇👇👇👇👇👇👇👇

"```TANZIA


✍️Kama una ndugu yako,  alopanda treni Kutoka dar, kwenda.

✍️Mpanda,  tabora,  mwanza -Kigoma.

✍️Treni imepata ajali maeneo ya Dodoma wilaya ya bahi.

✍️Mabehewa matano yameanguka,  na watu walokuwa kwenye Mabehewa hayo ma tano.

✍️Wote wamefariki,  chanzo cha ajali,  daraja limekatika.

✍️Tafadhali Sana share ujumbe huu,  kwa ndg jamaa na marafiki.

✍️Ili ndg wawasafiri wajue ndg yao Kama amesalimika."

                 👇👇👇👇👇👇👇👇👇 
 

Post a Comment

0 Comments