Zanzimana: Nusu Binadamu, Nusu Sokwe, Awashangaza Wazungu

 Zanzimana: Nusu Binadamu, Nusu Sokwe, Awashangaza Wazungu


 Kuna picha inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha mtoto au kijana mweusi tii wa Kiafrika, anayefananishwa sura yake na nyani au sokwe.

Anaonekana ni kijana mlemavu wa utindio wa ubongo, lakini umeshajiuliza kijana huyu ni nani na kwa nini yupo hivyo?

 

Chombo kimoja cha habari cha kimataifa kimefunga safari kutoka Ulaya kuja Afrika kumtafuta kijana huyu na sasa habari yake imeenea sehemu kubwa ya Dunia hii na sasa wanamfahamu. Kama kawaida yao wapo baadhi ya wazungu wapuuzi wanaokwenda kumtazama mtoto huyu kama kivutio.

Pia Zanzimana anapenda kula majani, matunda na mizizi na ana tabia zote za nyani au sokwe. Miaka ya nyuma Zanzimana alisababisha tafrani mno kwenye jamii yake ambayo ilitaka kumkataa na kumuona siyo binadamu wa kawaida huku wakimuona kama ishara mbaya au mkosi kwa jamii.

Ambacho wengi hawakijui ni kwamba, wazazi wa Zanzimana waliishi miaka mingi bila kupata mtoto na mara zote walimuomba Mwenyezi Mungu awape mtoto hata kama atakuwa wa ajabu huku wakisikitishwa na habari za wanawake kariba ya Bi Rukia za kutupa watoto!


Akiishi kwenye nchi kama Rwanda, kijana Zanzimana anapita kwenye nyakati tofautitofauti hasa za kibaguzi na watu kumtembelea kama watembeleavyo mbuga za wanyama, lakini mama yake hajawahi kumuacha
Mama yake anasema yeye na mumewe walifikia hatua ya kumuomba Mungu usiku na mchana awape mtoto hata kama atakuwa wa ajabu kwa sababu walitafuta mtoto kwa muda mrefu na kila aliposhika mimba iliharibika na alishajifungua watoto watano wakiwa wamekufa.

 

Mama huyo anasema kuwa, Zanzimana ni uzao wake wa sita ambao yeye na mumewe walimuomba Mwenyezi Mungu awape ‘japo mtoto mmoja hata kama ni wa ajabu ilimradi tu anaishi na wao wamepata uzao’.

Baada ya kubeba ujauzito kwa miezi tisa na ushee, mwaka 1999 alijifungua mtoto huyo.

 

Anasema alipomuona mwanaye baada ya kujifungua kuna kitu kilijitokeza kiasi cha kumshangaza. Anasema aliona mtoto aliyejifungua kuwa ni wa tofauti hivyo aliogopa kidogo, lakini akakumbuka maombi yake na mumewe kwa Mwenyezi Mungu kwamba, awape japo mtoto hata kama atakuwa ni wa ajabu!Anasema wao kama wazazi walikubaliana kumkuza mtoto wao huyo kwa kuwa yu hai.

 

Kuhusu kuongea, madaktari walimweleza mama yake mara tu baada ya kujifungua kwamba Zanzimana hataweza kuzungumza na kweli hadi sasa ana umri wa miaka 21 na hawezi kuongea.

 

Zanzimana hawezi kuongea kwa sababu hawezi kuongea kwa mujibu wa madaktari.Hawakuweza kumpeleka shuleni kwa sababu walielezwa kwamba kichwa chake hakiwezi kupokea elimu ya darasani, badala yake inashika vitu vya msituni na anafurahia maisha ya kukimbiakimbia mwenyewe msituni.

 


Mama yake anasema kuwa, amekuwa akimlisha Zanzimana nyasi kama ng’ombe au mbuzi na muda wake mwingi ni kufukuzana naye msituni ili kumrejesha nyumbani.

 

Zanzimana hajawahi kukanyaga darasani kama watoto wengi na kuna uwezekano asikanyage kabisa kama hatatokea msamaria-mwema wa kumpeleka kwenye shule maalum.Lakini kizuri kinachompa matumaini mama yake ni uwezo wa Zanzimana kupunga mkono kama ishara ya mawasiliano, jambo ambalo zamani alikuwa hafanyi hivyo.

 

Kwa jumla Zanzimana hana tabia kama binadamu wengine. Kwa uchungu, mama huyo anasema kinachomuuma ni watu na majirani kumuita mwanaye huyo nyani au sokwe.

 

Anasema kama mzazi, anaumia mno, lakini yote ameamua kumwachia Mwenyezi Mungu.

Anaamini kwamba watu wote wanaweza wakawatenga, lakini kamwe hataacha kumlinda mwanaye huyo. Hapa kuna somo kubwa mno kwamba, hata kama watu wote watakuacha, usitoke kwenye reli hasa kama unachokisimamia unakiamini!Post a Comment

0 Comments