Rais Wa Ufaransa Emmanuel Macron Akutwa Na Corona


 Taarifa kutoka ofisi ya Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron(42) zimesema kuwa amekutwa na virusi vya corona.

Macron alifanya vipimo mara tu alipoanza kujisikia daalili na sasa anajitenga kwa muda wa siku saba, taarifa kutoka Ikulu zimeeleza.

Zimeongeza kuwa, Macron bado anaendelea na shughuli za kuiongoza nchi hiyo huku akiwa amejitenga.

Wiki hii, Ufaransa iliweka marufuku ya watu kutotembea muda wa usiku baada ya maambukizi ya Corona kuongezeka.

Post a Comment

0 Comments