Uchaguzi wa Marekani 2020: Trump, Biden Wachuana Vikali


 Wamarekani wamepiga kura kumchagua rais katika uchaguzi ulioligawanya taifa hilo kwa kiwango kisichokuwa na kifani.

Matokeo ya awali ya urais nchini Marekani kati ya Donald Trump na hasimu wake wa Democrat Joe Biden yanaonesha mchuano kuwa mkali katika majimbo kadhaa.

 

Biden anaongoza akiwa na kura 224 za wajumbe wa majimbo na Trump ana 213.

Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa Biden ameshinda kwenye majimbo ya Virginia, Delaware,Vermont Connecticut, Illinois, Maryland, Massachusetts, New Jersey na Rhode Island huku Trump akiyanyakua majimbo la Florida, Texas, Virginia magharibi, Kentucky, na South Carolina, Alabama, Mississippi, Oklahoma na Tennessee.

 

Donald Trump anaongoza katika jimbo la Florida kwa karibu kura zote zilizohesabiwa.

Lakini majimbo mengine ya Georgia, Pennsylvania, Wisconsin, Michigan, Arizona, Ohio,  na North Carolina chochote kinatarajiwa.

 

Bunge la wawakilishi linatarajiwa kuwa katika mikono ya Democratic.

No comments