Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 3.11.2020


 Manchester City inaweza kumpa ofa mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi, 33, ya mkataba wa awali mwezi Januari kabla ya kuhamia England msimu ujao. (Daily Telegraph)

Manchester City wanajiandaa kumfanya mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 25 na kiungo wa kati wa Kibelgiji Kevin de Bruyne,29 kuwa wachezaji wanaolipwa pesa nyingi zaidi katika ligi ya Primia. (90 Min)

Atletico Madrid imeingia katika ushindani na Bayern Munich na Sevilla zikimfuatilia kwa karibu beki wa kulia wa Brighton Tariq Lamptey, 20. (Mail)

Nigeria

Manchester United, Leicester na Everton wangependa kumnasa winga wa Nigeria anayekipiga Villarreal Samuel Chukwueze, 21. (90 Min)

Paris St-Germain itakuwa makini katika uhamisho wa mchezaji wa England anayekipiga Tottenham Dele Alli,24, ikiwa atapatikana mwezi Januari. Klabu hiyo ya ufaransa ilifanya majaribio matatu yaliyogonga mwamba ya kumsajili kwa mkopo kiungo huyo wa kati msimu huu. (Mail)

Barcelona imeongeza nia yake ya kumnasa mshambuliaji wa Benfica na Uruguay Darwin Nunez,21, kama mbadala wa muda mrefu wa Luis Suarez.

Mchezaji huyo,33 aliondoka Barca kwenda Atletico Madrid mwezi Septemba. (ESPN)

Barcelona itatoa ofa mpya ya pauni milioni 7 kwa mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Uhispania Eric Garcia mwezi Januari.

Mchezaji huyo,19 anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu, Barca ikipendelea kumsajili. (Mirror)

kocha

Kuacha kibarua cha urais wa Barcelona kwa Josep Maria Bartomeus kunaweza kufanya mpango wa uhamisho wa Garcia au mshambuliaji wa Lyon Mamphis Depay, 26 kuwa mgumu mwezi Januari. (Marca)

David Alaba, 28, ameikosoa Bayern Munich baada ya kugundua kuwa klabu imeondoa ofa yao ya mkataba mpya. Mkataba wa mchezaji huyo wa nafasi ya ulinzi utakwisha mwishoni mwa msimu huu. (Mail)

Paris St-Germain ilitaka kumsajili Thiagi Alcantara,29, msimu huu lakini badala yake iliishia kwa kaka yake Rafinha,27, baada ya kiungo huyo wa kati kuondoka Bayern Munich kwenda Livepool. (France Football)

m

Kocha wa Inter Milan Antonio Conte, 51 amesema alikacha mara mbili nafasi ya kuifundisha Real Madrid kwakuwa hakutaka kuchukua jukumu hilo kwa timu ambayo tayari ilishauanza msimu wake. (Marca)

Kocha mkuu wa Brighton Graham Potter amemuacha mfungaji bora Neal Maupay,24, katika mechi dhidi ya Tottenham siku ya Jumapili kwa kuwa mshambuliaji huyo ana tabia isiyopendeza (Daily Telegraph)

No comments