Mzee aliefariki mwaka jana afukuliwa akutwa anapumua, hajaoza (+video)


 Ni mwezi mmoja uliopita ambapo wananchi katika Vijiji vya Umuoji na Amucha Mjini Imo Nigeria walipatwa na mshtuko wa karne baada ya kuifukua maiti ya mwanaume mmoja aliyefariki mwaka mmoja nyuma na kuikuta haijaharibika na bado inapumua.

Katika video inayoonyesha tukio hilo mwananchi mmoja alisikika akitoa ushuhuda kuwa mwanaume huyo alifariki na kuzikwa November 20, 2019 na kaburi lake lilifukulikwa Oktoka 8 mwaka huu kwa ajili ya kuzikwa upya.

Wananchi hao walitoa maelezo kwamba sababu ya mwili wa mwanaume huyo kufukuliwa na kutaka kuzikwa upya ni kutokana na shamba alilokuwa amezikwa kutokuwa lake wala la ndugu zake, hivyo mmiliki wa shamba hilo alihitaji kaburi hilo litolewe ndipo kioja hicho kilipotokea.

No comments