Watu 69 wauawa wakati wa maandamano Nigeria

Watu 69 wauawa wakati wa maandamano Nigeria

Rais wa Nigeria Muhammad Buhari amesema watu 69 wameuawa kwenye maandamano dhidi ya ukatili wa polisi, maandamano yanayofanyika nchini humo.

Waliouawa ni raia, maafisa wa polisi na wanajeshi, alieleza.

Shirika la Amnesty International lilisema mwanzoni mwa wiki hii kuwa takribani watu 56 wamepoteza maisha tangu yalipoanza maandamano, ikiwemo waandamanaji 12 waliouawa jijini Lagos siku ya Jumanne.

Kundi ambalo limekuwa mbele katika kuratibu maandamano sasa limewataka watu kubaki majumbani mwao.

Umoja wa wanaharakati wa wanawake pia umewataka watu kufuata masharti ya muda wa kuwepo majumbani yatakayowekwa kwenye majimbo yao.

Mitaa ya mji mkubwa wa Nigeria, Lagos yalikoanzaia maandamano hayo, imekuwa kimya lakini hali ya hofu imeendelea kuwepo.

Maandamano yalianza tarehe 7 mwezi Oktoba huku vijana wakidai kuvunjwa kwa kikosi cha polisi cha SARS.

Mmoja wa waandamanaji nchin Nigeria

Kikosi hicho kilivunjwa siku kadhaa baadae, lakini maandamano yameendelea.

Yalishika kasi baada ya mashambulizi ya siku ya Jumanne baada shirika la Amnesty International kusema kuwa vikosi vya usalama vimewaua watu karibu 12.

Jeshi la Nigeria limekana kuhusika katika tukio hilo.

Rais Buhari ametangaza idadi ya waliopoteza maisha katika mkutano na viongozi wa zamani wa Nigeria siku ya Ijumaa. Amesema kuwa miongoni mwa waliopoteza maisha raia ni 51, polisi 11 na wanajeshi saba.

Usiku wa jana, rais altoa hotuba fupi kwa njia ya televisheni akiwataka waandamanaji kusitisha maandamano na badala yake washirikiane na serikali ''kutafuta suluhisho''.

Rais Buhari alikosolewa kwa kutozungumzia mauaji.

 

No comments