Wahamiaji 140 Wapoteza Maisha Boti Ikizama


 WATU wapatao 140 wamepoteza maisha baada ya meli iliyokuwa na wahamiaji wapatao 200 kuzama katika pwani ya Senegal.

 

Katika taarifa yake, Ofisi ya Uhamiaji ya Kimataifa (IOM) imesema ajali hiyo ya meli ni mbaya zaidi kurekodiwa mwaka huu.

 

Chanzo cha ajali hiyo ni moto uliotokea katika meli hiyo saa kadhaa baada ya kuondoka ambapo  taarifa zinasema ulianzia kwenye mapipa ya kutunzia mafuta, jambo lililosababisha boti hiyo kupinduka na kuzama.

 

Mnamo Agosti mwaka huu, Umoja wa Mataifa ulizitakanchi kuhakiki upya nyendo za uhamiaji wa watu wao kwenda Ulaya kupitia Bahari ya Mediterranea kufuatia vifo vya wahamiaji 45 katika pwani ya Libya, tukio ambalo lilikuwa baya zaidi kwa mwaka huu wa 2020.

 

Mapema wiki hii, Serikali ya Senegal ilionya juu ya kuibuka tena kwa wahamiaji wanaojaribu kwenda Ulaya kupitia njia hatari mashariki mwa Bahari ya Atlantiki.

No comments