Waandamanaji 'wauawa kwa risasi' jijini Lagos - Nigeria

 

Watu kadhaa walioandamana dhidi ya polisi wakatili wameripotiwa kupigwa risasi na kufa na huku wengine wakiwa wamejeruhiwamjini Lagos, Nigeria.

Walioshuhudia tukio hilo wameiambia BBC kuwa wameona miili ipatayo 20 ilikuwa imetapakaa na wengine 50 wamejeruhiwa baada ya wanajeshi kufyatua risasi.

Shirika la kimataifa la Amnesty limesema limepata habari za kuaminika kuhusiana na vifo hivyo.

Maafisa wameahidi kufanya uchunguzi kuhusu shambulio hilo.

Amri ya kutotoka nje ndani ya saa 24 imewekwa mjini Lagos na miji mingine.

Waandamanaji sasa wamezunguka vituo vya polisi , kikosi maalum cha Sars, kimekuwa kikiendelea kwa muda wa wiki mbili .

Kutokana na mapigano ya risasi yanayoendelea , aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Marekani bi. Hillary Clinton amemtaka rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kuacha kuwaua vijana asitishe maandamano ya Sars.

#EndSARS ".

Mcheza mpira Nigeria Odion Jude Ighalo, ambaye anaichezea Manchester United, ameishutumu serikali ya Nigeria kwa kuua wananchi wake.

Alisema hayo kupitia ukurasa wa tweeter kwa kuweka video.

Tunafahamu nini kuhusu mapigano hayo?

Walioshuhudia tukio hilo walizungumzia wanaume ambao hawakuwa katika sare ambao walipiga risasi jioni ya siku ya Jumanne.

  Askari wenye silaha walikuwa wakiwazuia waandamanaji kabla ya risasi kuanza kupigwa , mwandishi wa BBC Nigeria Nayeni Jones anaripoti.

  Video katika mitandao ya kijamii ilikuwa ikionesha tukio hilo mubashara.

  Gavana wa jimbo la Lagos Babajide Sanwo-Olu akiwatembelea hospitalini watu waliojeruhiwa

  Shuhuda ambaye hakutaka jina lake kutajwa aliiambia BBC kuwa majira ya saa moja kasoro usiku walianza kupiga risasi katika maandamano ambayo yalikuwa ya Amani.

  Walikuwa wanapiga risasi moja kwa moja kwetu, lilikuwa tukio baya . Kuna mtu alipigwa risasi na kufa hapo hapo.

  Walipiga risasi kwa muda was aa moja na nusu na baada ya hapo askari walichukua miili ya waliouawa.

  Askari walikuwa wameweka zuio kwa waandamanaji hivyo magari ya wagonjwa yalishindwa kufika katika eneo la maandamano.

  Askari walikuwa wameweka zuio kwa waandamanaji hivyo magari ya wagonjwa yalishindwa kufika katika eneo la maandamano.

  Watu wengine wanne walioshuhudia waliiambia Reuters news agency kuwa askari waliwapiga risasi waandamanaji .

  Mmoja wao Alfred Ononugbo, 55, alisema: "Walianza kupiga risasi katika mkusanyiko huo .

  Niliona risasi zikipiga watu wawili.

  Katika ujumbe wa twitter wa Amnesty International Nigeria wamesema kuwa wana ushahidi tosha unaoonesha polisi wakitumia mabavu dhidi ya waandamanaji mjini Lagos".

  Msemaji wa Amnesty International Isa Sanusi alisema wana video inayoonesha polisi wakiwaua wananchi, wanajaribu kuhakiki ni wangapi.

  Je ni nini tunachofahamu kuhusu ufyatuaji huo wa risasi?

  Mashahidi walizungumzia kuhusu maafisa wa polisi waliovalia sare za polisi wakifyatua risasi katika makaazi ya watu matajiri ya Lekki siku ya Jumanne.

  Wanajeshi walionekana wakiweka vizuizi katika eneo la maandamano kabla ya ufyatuaji huo wa risasi, kulingana na mwandishi wa BBC Mayen Jones.

  Waandamanaji mjini Lagos waliweka vizuwizi na kufunga barabara katika mji huo mkubwa wa kibiashara
  Maelezo ya picha,

  Waandamanaji mjini Lagos waliweka vizuwizi na kufunga barabara katika mji huo mkubwa wa kibiashara

  Video zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zikiwa mubashara kutoka eneo hilo ziliwanonesha waandamanaji wakishughulikia waliojeruhiwa.

  Shahidi ambaye hakutaka jina lake litajwe aliambia BBC kwamba muda mfupi kabla ya saa moja wanajeshi walikongamana na kuanza kuwafyatulia risasi waandamanaji waliokuwa wakiandamana kwa amani moja kwa moja.

  ''Walikuwa wakifyatua risasi na kutukaribia . Zilikuwa ghasia. Mtu mmoja alipigwa risasi mbele yangu na kufariki papo hapo'', alisema.

  Mashahidi wanne waliambia Reuters wanajeshi waliwafyatulia risasi waandamanaji.

  Mmoja wao Alfred Ononugbo , mwenye umri wa miaka 55 alisema: Walikuwa wakifyatua risasi katikati ya waandamanaji . Niliona risasi zikiwapiga watu wawili.

  Gazeti la Premium Times liliwanukuu mashahidi wakisema kwamba takriban watu 12 waliuawa. Katika ujumbe wa Twitter,Shirika la Amnesty International Tawi la Nigeria lilisema limepokea ushahidi wa kweli lakini unaogofya kuhusu utumizi wa nguvu kupitia kiasi uliosababisha vifo vya waandamanaji katika lango la Lekki mjini Lagos.

  Msemaji wa Amnesty International Isa Sanusi baadaye alisema: Watu waliuawa na vikosi vya usalama katika lango la makaazi ya Lekki tunajaribu kuchunguza ni wangapi.

  Je utawala umejibu vipi?

  Katika taarifa siku ya Jumatano, rais Buhari hakuzungumzia moja kwa moja kuhusu ufyatuaji huo wa risasi lakini akawataka raia kuwa na subra huku mabadiliko ya kitengo cha maafisa wa polisi yakiendelea.

  Taarifa iliotolewa na ofisi yake ilisema kuvunjwa kwa kitengo cha SARS ilikuwa hatua ya kwanza katika mkusanyiko wa sera za mabadiliko ambazo zitahakikisha kuwepo kwa mfumo wa kitengo cha polisi kinachowajibika kwa raia wa Nigeria.

  ''Rais anataka kusisitiza kwamba serikali yake iko tayari kuweka mabadiliko katika kitengo cha polisi nchini Nigeria,''iliongezea.

  Mmoja wa waandamanaji mjini Lagos Nigeria Picha: 20 October 2020

  Jeshi hatahivyo halijatoa taarifa kuhusu matukio ya Lekki , lakini katika jumbe kadhaa za mtandao wa Twitter lilielezea ripoti za vyombo vya habari kama 'habari bandia'.

  Gavana wa Lagoz Babajide Sanwo-Olu, aliyetembelea hopsitali siku ya Jumatano alisema kwamba takriban watu 25 walijeruhiwa katika kile kinachoelezewa kama ufyatuaji wa risasi ambao haikuhitajika.

  ''Ni vyema kwamba hatujarekodi kifo chochote licha ya madai yanayosambaa katika mitandao ya kijamii'', alisema, akiongezea kwamba uchunguzi umeagizwa kufanyika.

  Je kumekuwa na wito gani mwingine?

  Aliyekuwa waziri wa masuala ya kigeni nchini Marekani Hillary Clinton amemtaka rais Buhari na jeshi kuacha kuwaua vijana wanaoandamana wa vuguvugu la #EndSARS ".

  Na aliyekuwa makamu wa rais nchini Marekani ambaye ndio mpinzani mkuu wa rais Donald Trump katika uchaguzi wa mwezi ujao Joe Biden - pia ametoa wito kwa mamlaka kusitisha ghasia dhidi ya waandamanaji.

  ''Marekani lazima iwaunge mkono raia wa Nigeria ambao wanaandamana kwa amani wakitaka mabadiliko katika kitengo cha maafisa wa polisi mbali na kukabiliana na ufisadi katika taifa lao'', alisema aktika taarifa.Mchezaji wa Nigeria Odion Ighalo, anayeichezea timu ya Man united aliishutumu serikali ya Nigeria kwa kuwaua raia wake wenyewe.

  ''Ni aibu kwa serikali hii'' , alisema katika video iliochapishwa katika mtandao wa twitter.

  No comments