Trump na Obama warushiana vijembe wakati wa kampeni

Trump na Obama warushiana vijembe wakati wa kampeni


 Katika kampeni za Democratics anayewania nafasi ya urais akiwa Joe Biden huko Pennsylvania, Bwana Obama alimuhusisha Trump na mjomba ambaye amechanganyikiwa na kusema kuwa ana ubaguzi wa rangi.

North Carolina, katika kampeni za Republican rais alimkebehi Obama kwa kukosea katika uchaguzi wa mwaka 2016 .

Huku siku 13 zikiwa zimesalia kufikia siku ya uchaguzi ,Bwana Biden anaonekana bado anaongoza katika kura za maoni.

Lakini ni kiwango kidogo sana kwa mapendekezo hayo kuwa uhalisia, matokeo ya kuamua nani atakuwa rais yatajulikana Novemba 03.

Wamarekani wengi wanaonekana kuwa wanapiga kura ya maoni kwa wingi mwaka huu, mpaka sasa tayari kura milioni 42 za maoni zimepigwa.

Trump alisema nini?

Katika kampeni zake Bwana Trump alimshambulia mpinzani wake wakati wote.

Alisema ni maamuzi ya wapiga kura kuchagua kati ya "Trump ili wapone kabisa " au "Biden waingie kwenye msongo wa mawazo".

Donald Trump hakuweza kuvumilia kutoimshambulia Barack Obama
Maelezo ya picha,

Donald Trump hakuweza kuvumilia kutoimshambulia Barack Obama

Bwana Biden alipumzika wiki nzima kwa ajili ya kujiandaa na majadala wa mwisho wa marais utakaofanyika usiku wa Alhamisi huko Nashville, Tennessee, wakati Trump akiwa anaendelea na kampeni katika majimbo ya pembezoni.

Rais hakusita kuingilia kati kampeni aliyoifanya Obama, kwa mara ya kwanza tangu kampeni hizo zianze mwezi Agosti.

"Hakukua na mtu yeyote ambaye alifanya kampeni kubwa kama Hillary Clinton zaidi ya Obama, si ndio?" Bwana Trump aliwaambia walioshiriki mkutano huo, alikuwa kila mahali.

Rais aliongeza: "Nadhani mtu ambaye hakuwa na furaha wakati Hillary aliposhindwa alikuwa Barack Hussein Obama."

Bwana Trump alimkejeli tena Obama kusema kuwa Bwana Biden hakuwa na vigezo vya kuwa rais, alipokua makamu wa rais mwaka 2009-2017.

Mwaka 2016, Bwana Obama aliripotiwa kuwa alimweka kando Biden kuwania nafasi ya urais na kumpa nafasi Hillary Clinton akiamini kuwa alikuwa anaweza kumshinda Trump.

Mwaka jana Obama alisema kuna uhitaji wa kuwa na mtu mpya katika uongozi wa Democratic, taarifa ambayo ilitafsiriwa kuwa hamkubali Biden.

Obama alisema nini?

Baada ya kumshambulia Bwana Trump namna alivyokabiliana na virusi vya corona na uchumi, Bwana Obama aligeukia mkutano wa Philadelphia kuhusu ujumbe wa Twitter wa rais.

Kura ya maoni inaonesha kuwa Joe Biden bado anaongoza
Maelezo ya picha,

Kura ya maoni inaonesha kuwa Joe Biden bado anaongoza

Alisema ikiwa Bwana Biden atashinda, "hatutakuwa na rais ambaye anatukana yeyote asiyemuunga mkono, au kutishia wengine kwa kuwapeleka gerezani. Hiyo sio tabia ya kawaida kwa rais".

Bwana Obama - ambaye bado ni miongoni mwa watu mashuhuri katika chama cha Democratic - alisema wapiga kura hawatavumilia tabia kama hizo kutoka kwa mmoja wa familia yao, "isipokuwa pengine kwa mtu asiyekuwa na akili timamu kwengineko".

"Kwanini watu wanatafuta visingizo kwa hilo?" alisema. "Oh, huyo ni yeye tu. Hapana!

"Wanahamasisha wengine kuwa wakatili. Na kugawanya watu. Na kuendeleza ubaguzi. Na huko kunaharibu jamii yetu."

Aliongeza: "Tabia ni muhimu. Sifa ya mtu ni muhimu pia."

Kuhusu janga la corona, Obama alizungumzia hatua za hivi karibuni za Trump kuhusu Covid-19: "Donald Trump hawezi kutulinda sisi. Yeye mwenyewe.

No comments