Tetesi za soka Ulaya Jumatano 28.10.2020


 Manchester United itaelekeza nguvu zake kutaka kumsajili beki wa RB Leipzig mfaransa Dayot Upamecano, 22, katika dirisha lijalo la msimu wa joto. (Times)

Liverpool ni klabu ya hivi karibuni kumfuatilia kiungo wa Iceland wa chini ya miaka 21 Isak Bergmann Johannesson, 17, ambaye anachezea IFK Norrkoping ya nchini Sweden. (Expressen - in Swedish)

Johannesson pia anawindwa na vilabu vya Manchester United na Juventus. (Aftonbladet - in Swedish)

Ansu-Fati-lying-on-pitch.

Juventus ilijaribu kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na Hispania forward Ansu Fati, 17, katika dirisha la usajili la majira ya joto lililopita. (Calcio Mercato - in Italian)

Brighton wamempatia beki wa pembeni wa England chini ya miaka 21, Tariq Lamptey, 20, mkataba mpya licha ya kuhusishwa na Bayern Munich. (Sun)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, atatrimkia Real Madrid katika dirisha lijalo la usajili la majira ya joto, kwa mujibu wa mchezaji mwenzake wa zamani wa timu ya taifa ya vijana ya Ufaransa chini ya miaka 21, Adil Rami (Metro)

Mchezajki wa Borrusia Dortmund,Jadon Sancho

Meneja wa Borussia Dortmund Lucien Favre anaamini kwamba uvumi kumuhusu winga Jadon Sancho kuelekea Manchester United ungeweza kusababisha kushuka kwa kiwango kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye miaka 20. (Mirror)

Mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez, 23, hajui nini kitatokea kuhusu mustakabali wake lakini kwa sasa yuko na furaha Inter Milan. (AS - in Spanish)

Winga wa Manchester City raia wa Algeria Riyad Mahrez, 29, yuko tayari siku moja kurejea Ufaransa kuchezea klabu yake ya utotoni Marseille. (Sun)

Barcelona itajaribu kumsajili mshambuliaji wa PSV Eindhoven na Uholanzi Donyell Malen, 21, kama itashindwa kukamilisha usajili wa Memphis Depay. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Mlinda mlango wa Manchester United, 33, Muargentina Sergio Romeroamepewa ofay a kurejea Racing Club de Avellaneda, lakini itampasa akubalia kukatwa mshahara wake kwa kiwango kikubwa. (Star)

Klabu ya Championship Birmingham City ni miongoni mwa vilabu vinavyotaka kumsajili mshambuliaji wa Brazil, Alexandre Pato, 31.ambaye yuko huru (Calciomercato)

Mkurugenzi wa ufundi wa Arsenal Edu amempiku meneja Mikel Arteta katika kumsainisha Ghana Thomas Partey, 27, badala ya kiungo mfaransa mwenye miaka 22 kutoka Lyon, Houssem Aouar. (L'Equipe, via Express)

Arsenal inachuana na mabingwa wa Ufaransa PSG na mabingwa wa Italia Juventus katika kumsainisha Aouar. (Sun)

No comments