Tamko la Trump 'kulipua' bwawa laikasirisha Ethiopia


 Waziri mkuu wa Ethiopia amesema nchi yake "haitakubali vitisho vya aina yoyote" baada ya Rais Donald Trump kusema kuwa Misri inaweza kuharibu bwawa lenye utata la Nile.

Bwawa hilo kubwa linakabiliwa na mzozo unaohusisha nchi za Ethiopia, Misri na Sudan.

Bw. Trump alisema Misri haiwezi kuishi bila bwawa hilo na huenda "ikalipua" ujenzi huo.

Ethiopia inaohisi kuwa Marekani inapendelea Misri katika mzozo huo.

Marekani ilitangaza mnamo mwezi Septemba kwamba itaipunguzia msaada Ethiopia baada ya nchi hiyo kuanza kujaza maji hifadhi iliyopo nyuma ya bwawa hilo mwezi Julai.

Kwa nini kuna mvutanokuhusu ujenzi huo?

Misri, ambayo inategemea maji ya mto Nile kwa 80%, ina hofu kuwa bwawa hilo litaathiri mfumo wa usambazaji maji na kuifanya Ethiopia kuwa na mamlaka juu ya usambaaji wa maji ya mto mkubwa Afrika.

Kituo cha kuzalisha umeme hakitatumia maji bali bwawa hilo linalojengwa na Ethiopia litaathiri kwa kiwango kikubwa kasi ya mtiririko wa maji.

Ujenzi wa bwa hilo la thamani ya dola bilioni nne mashariki mwa Ethiopia utakuwa mradi mkubwa zaidi wa umeme barani Afrika.

Kasi ya itakayotumiwa na Ethiopia kujaza maji bwawa hilo utaongoza jinsi utaatiri vibaya Misri -Cairo inapendekeza shughuli hiyo ifanywe pole pole. Mchakato ambao unatarajiwa kuchukua miaka kadhaa.

Sudan, ambayo inapakana na Misri upande wa juu pia inahofia kupunguziwa maji.

Ethiopia, ambayo ilitangaza ujenzi wa bwawa hilo mwaka 2011, inasema kuwa inataka kutumia maji ya bwahilo kujiendeleza kiuchumi

Ujenzi huo ulianza mwaka 2011 kaskazini mwa Ethiopia ambapo maji yatakayotumika ni 85% ya maji yanayotiririka kutoka mto Nile.

Hata hivyo ujenzi huo umesababisha kuwepo kwa mzozo kati ya Misri na Ethiopia, huku Sudan pia ikihusishwa na sasa Marekani inajaribu kutatua mzozo huo. Lakini sasa majadiliano yanasimamiwa na Muungano wa Afrika.

Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema nini?

Waziri Mkuu Abiy Ahmed hakuangazia moja kwa moja tamko la Trump, lkaini ameonekana kulikejeli hatua ambayo imezua gumzo mitandaoni.

Aliapa kuwa Ethiopia itakamilisha ujenzi wa bwawa hilo.

"Ethiopia haitakubali vitisho vya aina yoyote," alisema. "Waethiopia hawajawahi kupiga magoti mbele ya maadui wao, lakini wanawaheshimu marafiki zao. Hatutafanya hivyo wala siku zijazo."

Vitusho vya aina yoyote kuhusu suala hilo "havina msingi, havifai na moja kwamoja vinakiuka sheria ya kimataifa".

Sudan inahofia - maji ya mito miwili ya Nile itakutana Khartoum
Maelezo ya picha,

Sudan inahofia - maji ya mito miwili ya Nile itakutana Khartoum

Trump aliingilia vipi suala hilo?

Rais alikuwa akizungumza kwa simu na Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mbele ya wanahabari katika Ikulu ya White House siku ya Ijumaa.

Mkutano huo ulifanywa baada ya Israel na Sudan kufufua uhusiano wa kidiplomasia mchakato uliongozwa na Marekani

Suala la bwawa pia lilipoibuka Trump na Bw Hamdok walielezea matumaini ya kupatikana kwa suluhisho la amani katika mzozo unaozunguka bwawa hili.

Lakini Bw. Trump pia alisema "Ni hali ya hatari sana kwa sababu Misri haitaweza kuendelea kuishi hiyo".

Aliendelea kusema: "Na nimesema na tena narudia kwa sauti - watalipua bwawa. Na lazima wafanye kitu."

Majadiliano yamefika wapi?

Bw. Abiy anashikilia kuwa majadiliano yamepiga hatua tangu Muungano wa Afrika ilipoanza kuwa mpatanishi

Lakini kuna hofu kwamba hatua ya Ethiopia kuanza kujaza maji bwawa hilo huenda ikalemeza matumaini ya kusuluhisha masuala muhimu, kama vile kitachotokea wakati wa ukame na jinsi ya kusuluhisha mizozo ya baadaye.

Ethiopia dam map

No comments