Ozil Atemwa Arsenal


 RIPOTI kutoka jijini London zimedai kuwa kiungo mshabuliaji wa Arsenal, Mesut Ozil, ameondolewa kwenye kikosi cha wachezaji 25 cha timu hiyo kinachoshiriki  Ligi Kuu ya England

Orodha rasmi inatarajiwa kuwasilishwa FA jioni ya leo ikimaanisha kuwa Ozil hataweza kuichezea timu hiyo kwenye mechi za ligi hiyo mpaka mwezi Februari 2021.  Pia, hivi karibuni alitemwa kwenye kikosi kitachoshiriki michuano ya Europa.

Ozil ndiye mchezaji anayelipwa mshara mkubwa zaidi ndani ya The Gunners na kocha Mikael Arteta ameonyesha kutomhitaji fundi huyo wa Kijerumani ambaye mkataba wake unamfikia tamati mwakani.

No comments