Orodha ya waigizaji matajiri zaidi duniani Mwaka 2020

Utafiti uliofanywa na Jarida la forbes kuhusu watu matajiri duniani na utajiri wao mwaka huu umeangazia watayarishaji filamu na mapato yao kwa mwaka.

Fahamu baadhi waliongia kwenye orodha ya kumi la kwanza la waigizaji matajiri duniani.

The Rock Johnson

'The Rock', muigizaji wa filamu Mmarekani mwenye asili ya Canada ndiye aliyevunja rekodi ya kuwa mwigizaji tajiri zaidi duniani mwaka huu ikiwa ni mwaka wa pili mfululizo, kulingana na orodha ya utajiri ya jarida la Forbes.

Pia inasemekana kwamba mapato yake ni dola milioni 87.5 kwa mwaka, makubaliano yake ya hivi karibuni yakiwa ni dola milioni 23 ya kufanya filamu na mtandao wa Netflix.

Dwayne Johnson alifuata nyayo za baba yake Rocky na kuwa bondia.

Alikuwa na mafanikio makubwa kwenye ubondia kabla ya kugeukia uigizaji, na kuwa nyota kwenye filami ya Scorpion King, Fast & Furious 6 na kampuni ya Jumanji.

Reynolds

.

Muigizaji Reynolds, mtengenezaji filamu wa Marekani ambaye mapato yake ni dola milioni 71.5 kwa mwaka, kulingana na jarida la Forbes.

Alitengeneza zaidi ya dola milioni 20 kutoka kwa filamu moja tu.

Filamu zake za hivi karibuni ni pamoja na Free Guy, The Croods: A New Age na The Hitman's Wife Guard.

Mark Wahlberg

Mark Wahlberg
Maelezo ya picha,

Mark Wahlberg

Mark ni mwigizaji wa Marekani, mchekeshaji na mtayarishaji filamu wa Hollywood.

Filamu moja aliyotengeneza imekuwa ya tatu kwa orodha ya zilizotazamwa sana katika mtandao wa Netflix.

Alitengeneza mamilioni ya madola kwenye filamu za vichekesho.

Mapato yake kwa mwaka yanasemekana kuwa dola milioni 58.

Akshay Kumar

.
Maelezo ya picha,

Akshay Kumar

Muigizaji wa India Akshay Kumar amekuwa miongoni mwa waigizaji 10 wanaolipwa vizuri zaidi duniani mwaka huu.

Akshay, mmoja wa waigizaji maarufu huko Bollywood, ameigiza zaidi ya filamu 100 katika kipindi cha miaka 30 iliyopita.

Mapato yake ni dola milioni 48.5 kwa mwaka.

Amekuwa muigizaji pekee wa India kuingia miognoni mwa waigizaji 10 matajiri duniani.

Utajiri wake mkubwa unasemekana kwamba umetokana na matangazo ya biashara kwa makampuni makubwa makubwa kote duniani.

Sasa hivi anafanyia kazi filamu inayofahamika kama Belbotom.

Akshay Kumar
Maelezo ya picha,

Akshay Kumar

Pesa za Akshay zinatokana na mikataba yake kwenye uigizaji na biashara za kibinafsi kunakojumuisha tuovuti ya maonesho inayojulikana kama "The End".

Muigizaji huyo kila wakati amekuwa mstari wa mbele akilinganishwa na waigizaji wengine, tajiri na mwenye ushawishi katka jamii.

Akshay pia ni wa 52 katika orodha ya watu mashuhuri ya Forbes.

Watengenezaji filamu wa Hollywood inasemekana kwamba wako mbioni kumjumuisha Akshay kwenye filamu zao.

10. Jackie Chan

.
Maelezo ya picha,

Jackie Chan

Muigizaji anayetoka Hong Kong, China na anafahamika kwa filamu zake za maudhui ya vita na vichekesho.

Alitengeneza zaidi ya filamu 5 mwaka jana na kupata mapato ya zaidi ya dola milioni 40.

Licha ya mapato yake ya juu kutokana na matangazo ya biashara, ndio mwigizaji wa pekee kutoka China kuwa miongoni mwa waigizaji matajiri zaidi duniani

 

No comments