Ticker

6/recent/ticker-posts

Advertisement

Mondi Aibuliwa Dini ya Shetani


 

MAPYA yameibuka na kila mtu anasema lake hasa upande wa mahasimu wake, lakini kubwa ni kuibuliwa kwa skendo nyingine matata inayomhusisha staa mkubwa wa muziki barani Afrika, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na dini mpya ya kishetani.

 

JUKWAA MOJA NA CHRISS BROWN

Skendo hii imeibuliwa mara tu baada ya Diamond au Mondi kulamba shavu la shoo kwenye jukwaa moja na wanamuziki wa levo ya dunia kutoka Marekani, Chris Brown, Rick Ross na wengine, jambo linaloonesha nyota yake kuzidi kung’ara.

 

DINI YA MIFUPA NA MAFUVU

Achana na ile skendo ya kuwa Freemason, lakini sasa imetajwa jamii nyingine ya siri ya Skulls and Bones Society (Jamii ya Mafuvu na Mifupa) ambayo ni dini nyingine ya shetani inayosemekana Mondi ni mwanachama wake, ndiyo maana mambo yake yanamuendea supa na siyo dizeli, kiasi cha kulamba shavu hilo kubwa na kuwaacha wenzake waking’aa macho.

 

TUJIUNGE NA MTAALAM

Mmoja wa wataalam anayejua undani wa masuala ya jamii za siri duniani anaeleza juu ya dini hiyo ya kishetani ambayo ndani yake kuna kuabudu mafuvu na mifupa ya watu fulanifulani waliokuwa na nyota zinazong’ara duniani. Huku akiomba hifadhi ya jina kwa dhana ya kuwaogopa watu hao, mtaalam huyo wa nyota jijini Dar anasema; “Skulls and Bones nayo ni jamii ya siri kama ilivyokuwa Freemason, lakini ina nguvu zaidi duniani.

 

UKOO WA BUSH

“Tofauti na Freemason iliyoanzia barani Ulaya, hii ya mafuvu na mifupa yenyewe ilianzia katika chuo kikuu kimoja kule Marekani na ndiyo maana wanachama wengi ni watu maarufu kama Ukoo wa Bush, wanasiasa, wasanii, wafanyabiashara na wengine wenye mafanikio katika tasnia mbalimbali.

“Lengo kuu la kuanzishwa kwake lilikuwa ni zuri tu kwa sababu mambo mengi ya siri ndiyo yenye mafanikio huku duniani ukilinganisha na yale yanayokuwa wazi au hadharani.

“Lengo lilikuwa ni kupinga imani za jadi, kupinga matumizi ya nguvu za giza, kupinga unyanyasaji na kupinga dola kubwakubwa duniani, lakini kwa siri sana. “Jamii hii ilianzishwa mwaka 1832 na watu wawili, William Huntington Russell na Alphonso Taft.

 

MAFUVU NA MIFUPA YA MASHUJAA

“Hawa jamaa walikuwa na kawaida ya kuiba mafuvu na mifupa ya watu maarufu na mashujaa na kuyahifadhi kwa ajili ya kuyaabudu na kuchukua nyota za watu hao.

“Kuna kisa kimoja cha mtu aliyeitwa Haryln Geronimo alifungua mashtaka akiwashtaki Skulls and Bones akiwahusisha na kuiba mabaki ya mtu shujaa aliyeitwa Geronimo ambaye alikuwa ni shujaa kutoka Jamii ya Apache (Red Indians).

“Miaka kadhaa imekuwa ikipigiwa kelele jamii hii ya Fuvu na Mifupa kuwa imeshikilia mabaki ya Geronimo ikiyatumia kwa shughuli zake za kiimani. “Mlalamikaji huyo alisema anaamini kabisa kutoka moyoni mwake, kuwa roho ya Geronimo haikuachiliwa.

 

“Wakongwe akina Bush na wengine ambao ni wanachama wa Skulls and Bones walichimba mabaki ya Geronimo kutoka kaburini, wakaiba fuvu na mifupa yake.

 

“Jamii hii ikachukua mabaki hayo na kuyaweka makao yao makuu.

 

“Kuna mambo mengi ambayo yamekuwa yakizungumzwa kuhusiana na jamii hii hasa kuwafanya wanachama wake kuwa na nguvu mno duniani.

 

“Ni imani ambayo nchi za huku kwetu haziifahamu sana, lakini kwa huko kwa wenzetu hasa Marekani ni kundi kubwa na la kutisha.

 

WAMO VIONGOZI, MASTAA WAKUBWA

“Ni jamii yenye viongozi wakubwa sana duniani na watu maarufu au mastaa hasa hawa wanamuziki wakubwa kama akina Kanye West, Beyonce, Jay –Z na wengine wengi. “Pia jamii hii inahusishwa na Kundi la Mafi a (jamii ya makundi ya kihalifu) kwa miaka hiyo. “Pia jamii hii ilipatikana katika vyuo vikuu mbalimbali duniani, lakini siku hizi hata kwenye vyuo vya kawaida wapo.

 

“Kwenye vyuo vikuu kuna elimu inaitwa; ‘The secret doctrine of hypothesis in science, religion and philosophy’. “Ukikutana na mtu haamini uwepo wa Mwenyezi Mungu, mara baada ya kutoka chuo, basi ujue Skulls and Bones wameshafanya yao.

 

“Ndivyo ilivyo hata kwa hawa wasanii wetu kama huyo Diamond na wengine huwezi kuwaona kwenye nyumba za ibada, sasa ukiona hivyo ujue lisemwalo lipo au laja.

 

SAHAU FREEMASON

“Kuhusu Skulls and Bones, sahau kabisa kuhusu Freemason. Hawa jamaa ndiyo jamii yenye nguvu zaidi duania hizo nyingine zinafuata. “Hivyo kama lisemwalo kuhusu Diamond ni kweli, basi watu wajiandae kuona mafanikio yake makubwa zaidi ya hizo shoo.

 

TAHADHARI KUBWA

“Lakini…kwenye jamii hii kuna tahadhari kubwa inapaswa kuchukuliwa kwa sababu wengi waliokuwa wanachama matajiri kwenye jamii hii waliishia kubaya.

“Hebu mkumbuke mtu kama Michael Jackson au kwa sasa hebu mtazame R Kelly anavyoteseka gerezani akiwa hoehae, wakati alikuwa alikuwa miongoni mwa wanamuziki matajiri duniani.

“Hakuna jambo lisilokuwa na ubaya wake, Skulls and Bones wanaweza kukupa utajiri na maisha ya kifahari, lakini ukweli huwa mambo haya hayadumu…”

 

MONDI NA MAFUVU

Kuna kipindi zilisambaa picha zikionesha fuvu lililodhaniwa ni la binadamu likiwa mezani ofi sini kwake na kuibua maswali mengi huku fuvu hilo likihusishwa na imani za kishetani.

 

“Hata mimi niliiona picha hiyo na ni kweli ni moja ya alama za hawa Skulls and Bones. Unajua fuvu la binadamu ni moja ya Alama za Skulls and Bones na kama unavyojua Diamond amekuwa akitajwatajwa kujiunga na jamii hiyo,” anasema mtaalam huyo.

 

MONDI ALIVYOJITETEA

Kwa upande wake Mondi alipoulizwa juu ya uwepo wa fuvu hilo lililodhani kuwa ni la binadamu ndani ya ofi si zake (wakati huo zikiwa Sinza-Mori jijini Dar), alijitetea; “Ni urembo tu au pambo kama mapambo mengine, hakuna kitu kama hicho.

 

“Usidanganyike, hakuna anayeweza kumuweka mtu juu zaidi ya Mwenyezi Mungu. “Mimi naswali sana na ninamtegemea Mungu kwa kila kitu na kweli ananipigania.

 

“Unajua watu wengi wamekuwa wakizungumza oooh…natumia uchawi, lakini ukweli ni kwamba maombi, ubunifu, juhudi na heshima ndivyo vitu vinavyoweza kumfanya mtu yeyote kupata mafanikio katika kitu akifanyacho au jambo alifanyalo.”

 

KUHUSU SHOO…

Mondi, Chris Brown na mastaa wengine wanatarajiwa kutumbuiza jukwaa moja kwenye Tamasha la Afro Nations litakalofanyika Julai, mwakani nchini Ureno. Orodha ya mastaa hao ilitangazwa mapema Septemba, mwaka huu baada ya kuahirishwa kutokana na janga la Corona.

 

Mbali na Chriss Brown, Mondi ambaye amekuwa akisifi ka kama msanii anayepeperusha vilivyo bendera ya Bongo Fleva, atakuwa na mastaa wengine kama Rick Ross na French Montana kutoka Marekani, Wiz Kid, Burna Boy, 2 Face Idibia, Tekno, Mr Flavour kutoka Nigeria, Koffee Olomide kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na wengine wengi.

Post a Comment

0 Comments

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();