Ticker

6/recent/ticker-posts

Advertisement

Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2020: John Magufuli atangazwa mshindi wa urais

 

Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2020: John Magufuli atangazwa mshindi wa urais

Magufuli ameshinda kwa kupata kura 12,516,252 ambayo ni asilimia 84 ya kura zote zilizopigwa.

Tundu Lissu kutoka chama cha upinzani cha Chadema ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 1,933,271 ya kura zote ziizopigwa.

Jumla ya watu 15,91950 walipiga kura hizo wakati waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 29,754,699 kwa mujibu wa Tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC).

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametetea nafasi yake baada ya kushinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumatano wiki hii.

"John Magufuli ndio mshindi wa uchaguzi , amepata kura nyingi halali kuliko wagombea wengine, amechaguliwa kuwa rais wa tanzania na Samia suluhu Hassan kuwa makamu wa rais,''Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Jaji Semistocles Kaijage ametangaza.

h

Ni rasmi sasa mgombea wa chama tawala nchini Tanzania CCM, John Pombe Magufuli amechaguliwa tena kwa ushindi wa kishindo.

Vyama vikuu vya upinzani hata hivyo tayari walishakataa matokeo ya uchaguzi wa siku ya Jumatano wakidai uligubikwa na udanganyifu.

Uchaguzi huu ambao Magufuli alikuwa akiwania nafasi hiyo ya juu alikuwa na washindani wengine 14.

Matokeo hayo yamemthibitisha Bwana Magufuli kutoka Chama Cha Mapinduzi akipata nafasi ya kuhudumu nafasi hiyo kwa miaka mingine mitano ya mwisho.

Post a Comment

0 Comments