Kiongozi wa Al-Qaeda Auawa Afghanistan


 ABU Muhsin al-Masri, Mmisri aliyechukuliwa kama kiongozi nambari mbili wa kundi la Al-Qaeda mwenye ushawishi zaidi katika kundi hilo katika kanda ya  India, ameuawa katika mkoa wa Ghazni katikati mwa Afghanistan, idara ya kitaifa ya usalama nchini Afghanistan imeandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Idara hiyo haikutoa maelezo zaidi juu ya oparesheni hiyo na hakuonyesha ni lini ilifanyika. Jina la Al-Masri liko kwenye orodha ya magaidi wanaotafutwa sana na shirika la upelelezi la FBI la Marekani.

 

Al-Masri alikuwa anatafutwa na  FBI nchini Marekani kwa kutoa ufadhili wa bidhaa na raslimali kwa shirika moja la kigeni linalohusika na ugaidi na pia kwa njama ya kuwaua raia wa Marekani.

No comments