Ticker

6/recent/ticker-posts

Advertisement

IGP Sirro Atoa Onyo La Mwisho Kuelekea Uchaguzi Kesho -Video


 MKUU wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro amesema kuna watu 42 waliokamatwa kisiwani Pemba wakidaiwa kuwashambulia polisi waliokuwa wakisambaza masanduku ya kura jana.

 

IGP Sirro amesema hayo leo Oktoba 27, 2020 jijini Dar es Salam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa za vikundi vya watu wanaotaka kufanya vurugu.

“Kama kule Zanzibar, wakati askari wanasambaza masanduku ya kupigia kura, kuna vijana walianza kurusha mawe na wameshulikiwa. Wapo karibu 42. Mpaka sasa hakuna kifo chochote,” amesema IGP Sirro.

Kuhusu upigaji kura, Siro alisema na  kuwa jeshi lake limejipanga vizuri kukabiliana na hali yoyote ya uvunjifu wa amani.

“Tumejipanga vizuri kuhakikisha hakuna uvunjifu wa amani. Kesho asubuhi kama ni mmoja wa wanaokwenda kupiga kura, nenda ukapige kwa sababu Jeshi la Polisi limejipanga vizuri,” alisema.

 

Amewaonya wanasiasa wanaohamasisha wananchi walinde kura, akisema watakumbana na nguvu ya jeshi hilo.

“Wanaolinda kura ni mawakala wao. Kila chama kimepeleka mawakala. Kuna baadhi ya vyama vinaona vimeshindwa, vinaanza kuleta uvunjifu. Sisi polisi tunasema atakayeshinda ndiye atakuwa kiongozi,” amesema.

 

Amewataka wadau, ikiwemo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na mawakala kutimiza wajibu wao ili kuepusha vurugu.

“NEC itimize wajibu wake, wasimamizi watimize wajibu, mawakala watimize Wajibu,” amesema.

Post a Comment

0 Comments