Dayna, Patoranking Uso kwa Uso Nigeria


 MREMBO anayefanya poa kunako gemu la muziki wa Bongo Fleva, Mwanaisha Nyange ‘Dayna Nyange’, hivi karibuni ameibua gumzo baada ya kuonekana katika picha ya pamoja na msanii toka nchini Nigeria Patrick Nnaemeka Okorie ‘Patoranking’.

 

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Dayna amesema kuwa ukaribu wake na msanii huyo ni kwa sababu ya kazi na sio vinginevyo na hivi sasa yupo nchini Nigeria kwa sababu ya kazi zake ambazo asingependa kuziongelea kwa kuwa bado muda muafaka haujafika.

 

“Hakuna lolote linaloendelea kati yangu na Patoranking, kuna kazi za muziki nimekuja kufanya huku Nigeria, lakini kwa sasa nisingependa kuziongelea sana kwa sababu bado mambo yapo jikoni, hivyo naomba mashabiki wakae mkao wa kula,” alisema Dayna.

No comments