Buibui hatari na anayeogopeka zaidi aonekana Uingereza


 Buibui hatari zaidi ameonekana kwa mara kwanza Uingereza.

Buibui huyu yuko kwenye orodha ya wadudu hatari zaidi na wanaogopwa nchini Uingereza.

Buibui wa aina hiyo ameonekana katika maeneo matatu pekee, huko Dorset na Surrey, na hawajawahi kuonekana tangu mwanzoni mwa mwaka 1990.

Mike Waite, ambaye alimgundua buibui huyo kupitia mafunzo ya wizara ya ulinzi katika eneo la Surrey, alisema alikuwa juu ya mwezi.

Mtafiti huyo alipata buibui ambao walikuwa hawajakuwa, baada ya kuwatafuta kwa kipindi cha miaka miwili.

Great Fox-Spider
Maelezo ya picha,

Buibui hatari aliyegunduliwa ana macho nane - macho mawili juu ya kicha , mawili mbele ya kichwa na macho manne karibu na mdomo.

Buibui huyo hatari, 'Alopecosa fabrilis',anaishi ardhini na anaonekana zaidi usiku.

Ni miongoni mwa buibui wakubwa zaidi katika jamii ya buibui.

Kwa mujibu wa taasisi ya wanyama pori ya Surrey Wildlife Trust, wamesifia kugunduliwa kwa buibui huyo wa ajabu mwenye macho meusi nane.

Bwana Waite, kutoka taasisi ya Surrey Wildlife Trust, alisema: "Nimeshagazwa sana kuona kuwa buibui huyu hatari bado yupo Uingereza.

"Ingawa nmekuwa nafuatilia sana juu ya buibui, Nnajivunia kwa kutoa mchango huu muhimu kwa wanaayansi.

Great Fox-Spider

No comments