Ben Pol Amfungulia Dunia Darasa


 DAR: Mkali wa Hip Hop Bongo, Shariff Thabeet ’Darasa’, amefunguka kuwa hadi hapo alipofikia, siyo yeye, bali ni sapoti ya msanii mwenzake, Bernard Paulo ‘Ben Pol’.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Darasa ambaye amekuwa akisifika kuwa na staili ya kitofauti kwenye uimbaji wake, ameweka wazi kuwa, kwenye orodha ya watu wake muhimu, hawezi kumsahau Ben Pol wala kumvunjia heshima kwani anamjua vizuri katika safari yake ya muziki.

 

“Najua watu huwa tunasahau fadhila na mimi kiukweli nisiwe mchoyo wa kutoa shukurani, ninamshukuru sana, Ben Pol kwa mambo aliyoweza kunifanyia mpaka hapa nilipofikia.

 

“Alikuwa mwalimu mzuri sana kwangu na alikuwa anapenda nitimize ndoto zangu, hakutaka nikate tamaa kabisa,” anasema Darasa.

Ben Pol Amfungulia Dunia Darasa Ben Pol Amfungulia Dunia Darasa Reviewed by Junior TV on October 26, 2020 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.